Kebo ya kusambaza umeme kutoka ufukweni hadi melini yaanza kufanya kazi huko Malta

人民网

      (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 11, 2024

      Vifaa vya mradi wa kusambaza umeme kutoka ufukweni hadi melini vikionekana Valletta, Malta, tarehe 10 Julai 2024. (Picha na Jonathan Borg/Xinhua)

      VALLETTA - Kutokana na mradi wenye thamani ya euro milioni 33 (dola milioni 36 za Kimarekani), meli za kitalii zinazotia nanga katika Bandari Kuu ya Malta zitaweza kuzima injini zao na kuunganishwa kwa umeme wa ufukweni, na hivyo kupunguza utoaji wa hewa chafu na uchafuzi wa mazingira kwa asilimia 90.

      Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi siku ya Jumatano, Waziri Mkuu wa Malta Robert Abela amesema kuwa ikiwa ni nchi ya kisiwa, bandari za Malta ndiyo kiini cha uchumi wake kwani zinahimiza biashara na utalii.

      Amesema, miradi kama vile kuunganisha umeme katika Bandari Kuu unaifanya nchi hiyo iwe mwanzilishi na kielelezo katika kutumia suluhu endelevu za baharini.

      Amesema mradi huo ni moja ya miradi bora zaidi ya aina yake barani Ulaya, na kuifanya Malta kuwa moja ya nchi za kwanza za kufunga vifaa vya usambazaji wa umeme kutoka ufukweni hadi melini vyenye uwezo wa kusambaza meli za kitalii hadi tano kwa wakati mmoja.

      Mradi huo, unaofadhiliwa kwa pamoja na Malta na mfuko wa Umoja wa Ulaya unaounganisha Kituo cha Ulaya, utaboresha kwa kiwango kikubwa ubora wa hewa kwa familia karibu 17,000 zinazoishi katika sehemu hiyo ya Malta.

      Mfumo huo unaweza kutoa jumla ya MVA 64 za umeme wa ufukweni. Inafanya kazi na voltages ya 11 kV au 5.5 kV na masafa ya 50 au 60 hertz, yanayosaidiwa na vituo vya kubadilisha mawimbi vyenye transfoma 18 na vibadilishaji vinne vya mawimbi, ambavyo vinasambaza umeme kwa kebo zenye urefu wa kilomita 90.

      Mradi huo unatarajiwa kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni (CO2) kwa tani takriban 30,400 kila mwaka.

1/6