Kituo cha kubadilisha umeme cha Zhongning chaendelea kujengwa huko Ningxia, Kaskazini mwa China

人民网

      (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 11, 2024

      Wafanyakazi wa Kampuni ya Ningxia ya Shirika la Gridi ya Taifa la China wakifanya kazi kwenye kituo cha kubadilisha umeme cha Zhongning, Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia, kaskazini-magharibi mwa China, Julai 10, 2024.

      Ujenzi wa kituo cha kubadilisha umeme cha Zhongning unaendelea ikiwa ni sehemu ya njia ya kusambaza umeme wenye voteji ya juu (UHV) yenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,600 kutoka Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia kaskazini magharibi mwa China hadi Mkoa wa Hunan, katikati mwa China.

      Mradi huo utasambaza umeme uliozalishwa kutoka kwenye vituo vya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo na jua katika jangwa la nne kwa ukubwa nchini China, Jangwa la Tengger.

      Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2025 na umeundwa kwa uwezo wake wa kila mwaka wa kusambaza umeme wa karibia kilowati-saa bilioni 36 hadi 40. 

      (Xinhua/Wang Peng)

1/9