Waziri Mkuu wa China afanya mazungumzo na waziri mkuu wa visiwa vya Solomon

人民网

      (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 12, 2024

      Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Visiwa vya Solomon Jeremiah Manele, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, mjini Beijing, China, Julai 11, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

      BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Visiwa vya Solomon Jeremiah Manele mjini Beijing siku ya Alhamisi, akitoa wito wa kuendelezwa zaidi kwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya pande hizo mbili kwa zama mpya.

      Li amesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka mitano iliyopita, uhusiano huo umedumisha maendeleo makubwa, ukiweka mfano wa ushirikiano wa Kusini-Kusini kati ya nchi zinazoendelea.

      Amesema, China inapenda kushirikiana na Visiwa vya Solomon ili kuimarisha zaidi msingi muhimu wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote wa kuheshimiana na maendeleo ya pamoja kwa zama mpya na kuboresha kila wakati ustawi wa watu wa nchi hizo mbili.

      Li amesisitiza kuwa China inaunga mkono watu wa Visiwa vya Solomon katika kuchagua njia ya maendeleo inayoendana na hali zao halisi za kitaifa, na inapenda kuendelea kuungana mkono kithabiti katika maslahi ya msingi ya kila mmoja wao.

      Amesema, China inapenda kutoa uzoefu zaidi wa maendeleo kwa Visiwa vya Solomon, na kuimarisha ushirikiano katika miundombinu, maendeleo ya vijijini, habari na mawasiliano na kuhamia kwenye maendeleo ya kaboni chache.

      Amesema China inatumai kuagiza bidhaa bora zaidi za kilimo na chakula kutoka Visiwa vya Solomon na kuhimiza kampuni za China kuwekeza katika Visiwa vya Solomon.

      Kwa upande wake Manele ameshukuru kwa uungaji mkono mkubwa wa China kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Visiwa vya Solomon.

      Amesema kuwa Visiwa vya Solomon vinashikilia kwa dhati kanuni ya kuwepo kwa China moja, vinaunga mkono maono ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu, Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) na mipango mingine mikuu mitatu ya kimataifa, inaunga mkono Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani, na kuthamini sana mchango muhimu wa China katika amani na maendeleo ya Dunia.

      Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Visiwa vya Solomon Jeremiah Manele, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, mjini Beijing, China, Julai 11, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

      (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)