-
Hezbollah yaapa kulipiza kisasi kwa Israel kutokana na kumuua kamanda wake wa kijeshi
BEIRUT - Kiongozi wa Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah ameapa siku ya Jumanne kufanya hatua kali za ulipizaji kisasi kutokana na mauaji ya kamanda wake mkuu wa kijeshi, Fouad Shokor, kituo cha televisheni cha nchini Lebanon cha al-Manar kimeripoti huku kikimnukuu akisema kuwa: "Hii ni vita kubwa, na damu ya watu wetu ni ghali sana. Mauaji hayatapita bila kulipiza kisasi." "Kulipiza kisasi kwetu kwa mauaji ya kamanda wetu bila shaka kunakuja, na kutakuwa kwa nguvu na chenye athari kubwa. Tunaweza
07-08-2024
-
Jeshi la Sudan lahamisha waumini 6 wa kanisa katoliki wa Italia kutoka Khartoum
KHARTOUM - Jeshi la Sudan (SAF) limetangaza siku ya Jumanne kuwahamisha waumini sita wa kanisa katoliki wa Italia na raia 20 wa Sudan Kusini ambao walikuwa wamekwama kusini mwa Khartoum tangu kuzuka kwa vita mwezi Aprili mwaka jana. "SAF na Idara kuu ya Ujasusi (GIS) imehamisha watawa watano wa Jumuiya ya Wakatoliki wa Italia, kasisi kutoka Jumuiya ya Don Bosco ya Italia, na raia 20 wa Sudan Kusini kutoka kusini mwa Khartoum," Nabil Abdalla, msemaji wa SAF amesema katika taarifa. Watu hao walioh
07-08-2024
-
Ukanda wa utamaduni wa China na Cambodia waingiza msukumo katika utalii wa kikanda
SIEM REAP, Cambodia - Ukanda wa Utamaduni wa China na Cambodia umezinduliwa siku ya Jumanne kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Angkor wa Siem Reap, kaskazini-magharibi mwa Cambodia, ukiingiza msukumo mpya kwenye maendeleo ya utalii wa kikanda. Ukiwa na kaulimbiu ya " Urithi wa Dunia Uso kwa Uso, Kufunzana kati ya Ustaarabu Mkono kwa Mkono," ukanda huo wa utamaduni unalenga kuhimiza zaidi uanuai wa utamaduni na mali ya urithi wa nchi hizo mbili kwani mwaka 2024 ni mwaka wa mawasiliano kati ya
07-08-2024
-
Rais wa Zambia atoa wito wa kufanyika makubaliano ya kimataifa kumaliza mgogoro kati ya Russia na Ukraine
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ametoa wito wa kuwepo kwa maelewano ya haraka ya kimataifa ili kumaliza mgogoro kati ya Russia na Ukraine. Amesema hayo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Ivanovych Kuleba ambaye anatembelea nchini Zambia. Amesema kuwa mgogoro wa Russia na Ukraine unahitaji kutatuliwa kwa njia za amani, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa ili kuongeza hali ya utulivu na amani katika eneo hilo. Aidha ametoa wito wa kuimarishwa kwa uhusiano wa pand
07-08-2024
-
Niger yatangaza kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine “mara moja”
Msemaji wa serikali ya kijeshi ya Niger Amadou Abdramane Jumanne ametangaza kupitia televisheni ya kitaifa akisema, Niger itavunja uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine “mara moja”. Kwenye taarifa yake amesema, wanachukua hatua hiyo kutokana na kitendo cha Ukraine cha “kuunga mkono makundi ya kigaidi”, na kutoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufanya uamuzi juu ya “uvamizi” wa Ukraine. Siku mbili zilizopita, serikali ya mpito ya Mali ilitangaza kuwa itavunja uhusiano wa kidiplomasia
07-08-2024
-
Quan na Chen wa China wanyakua medali za dhahabu na fedha katika fainali ya wanawake kupiga mbizi kutoka jukwaa la kimo cha mita 10 kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris
Kwenye fainali ya mchezo wa kupiga mbizi kwa wanawake kutoka jukwaa la kimo cha mita 10 ya Michezo ya Olimpiki ya Paris iliyofanyika jana Jumanne, mpiga mbizi wa China Quan Hongchan amenyakua medali ya dhahabu, huku mchezaji mwingine wa China Chen Yuxi akishinda medali ya fedha.
07-08-2024
-
Chebet wa Kenya ashinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 5000 kwa wanawake katika Michezo ya Olimpiki ya Paris
Mkenya Beatrice Chebet alifanya umalizaji wa kishindo ili kushinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 5000 kwa wanawake katika Michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Jumatatu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alivuka mstari wa mwisho wa mbio hizo kwa kumaliza mbio kwa dakika 14 sekunde 28.56, zaidi ya sekunde mbili mbele ya bingwa mtetezi Sifan Hassan wa Uholanzi, ambaye amepata medali ya fedha. Nadia Battocletti wa Italia amepata medali ya shaba kwa kumaliza mbio kwa dakika 14 sekunde 31.
07-08-2024
-
China yatoa wito kwa ICC kuheshimu kikamilifu mamlaka ya mahakama na masuala halali ya Sudan
UMOJA WA MATAIFA - Dai Bing, naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumatatu kuheshimu kikamilifu mamlaka ya mahakama na masuala halali ya Sudan wakati wa kushughulikia kesi ya Darfur. "China imekuwa ikifuatilia kwa karibu uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kuhusu hali ya Darfur," amesema Balozi Dai katika hotuba yake kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ICC Sudan. Balozi Dai a
06-08-2024
-
Zou Jingyuan ashinda medali ya pili ya dhahabu ya China ya mchezo wa Jimnastiki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris
PARIS - Zou Jingyuan alijitahidi kushinda jeraha la bega na kutwaa taji la jimnastiki za kisanii kwenye milingoti sambamba kwa wachezaji wa kiume siku ya Jumatatu na kuipatia China medali ya pili ya dhahabu ya jimnastiki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris ambapo bingwa huyo mtetezi Zou ni mchezaji pekee wa tatu duniani kushinda medali mbili za dhahabu mfululizo kwenye mashindano ya mchezo huo, akikusanya pointi nyingi 16.200 kumshinda Illia Kovtun wa Ukraine, ambaye alichukua medali ya fedha kw
06-08-2024
-
Mkandarasi wa China apata mafanikio ya kupitika kwa handaki la mwisho kwenye njia kuu ya usafiri wa haraka Nepal
KATHMANDU – Handaki la mwisho limefaulu kupasuliwa na kupitika siku ya Jumatatu kwa mradi wa pili ulio chini ya kandarasi ya kampuni ya China chini ya mradi wa ujenzi wa njia kuu ya usafiri wa haraka wa Kathmandu-Terai/Madhesh, ambapo Waziri Mkuu wa Nepal KP Sharma Oli ameuelezea kuwa ni "hatua muhimu" katika kufikia malengo ya maendeleo ya Nepal. Baada ya waziri mkuu kubonyeza kitufe, mlipuko wa mwisho ulilipuliwa na kupasua sehemu ya mwisho ya handaki la kushoto la Dhedre. "Kushuhudia mafaniki
06-08-2024