China yashuhudia ongezeko la watalii wa kigeni kufuatia sera za kuingia China bila visa kuunganisha ndege kwenda nchi zingine

人民网

      (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 11, 2024

      Watalii kutoka Uswizi wakijipiga picha ya pamoja mbele ya Jumba la Qiniandian, kwenye Hekalu la Tiantan mjini Beijing, China, Julai 9, 2024. (Xinhua/Ju Huanzong)

      BEIJING - Hivi sasa, raia wa kigeni kutoka nchi 54 wanastahiki sera za kuingia na kukaa China bila visa ili kuunganisha ndege kwenda nchi nyingine kwa saa 72/144 ambazo zimeanza kufanya kazi katika bandari 38 za maeneo 18 ya ngazi ya mikoa kote nchini China ambapo kufuatia hatua hizo kuanzishwa tangu Januari mwaka huu China imerekodi safari milioni 14.64 za watu wa kigeni wanaoingia nchini China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 152.7 mwaka hadi mwaka, Idara ya Taifa ya Uhamiaji ya China (NIA) imetangaza Julai 5.

      Kwa mujibu wa NIA, idadi ya maombi ya kuingia China bila viza zilizotolewa na raia wa kigeni ilizidi milioni 8.54 kuanzia Januari hadi Juni, ikichukua asilimia 52 ya safari zote za watu wanaoingia China na ikiwakilisha ongezeko la mwaka hadi mwaka la asilimia 190.1

1/8