Mkutano wa Afrika kuhusu uchumi wa bluu waanza nchini Kenya

人民网

      (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 05, 2024

Picha iliyopigwa Aprili 3, 2024, ikionyesha mandhari ya jiji la Nairobi, Kenya. (Xinhua/Han Xu)

      KWALE, Kenya – Mkutano wa pili wa Afrika kuhusu uchumi wa bluu umeanza huko Kwale, mji wa Pwani wa Kenya siku ya Jumatano, ukifuatilia zaidi mikakati ya kuhimiza uwekezaji katika sekta hiyo ya bara la Afrika.

      Mkutano huo wa siku mbili wa Wekeza Bluu Afrika 2024 umevutia mashirika zaidi ya 200 ya maendeleo, wawekezaji, wajasiriamali, na maafisa waandamizi wa serikali kutoka nchi 36 barani Afrika kuhudhuria kwenye mkutano huo.

      Salim Mvurya,Waziri wa Madini, Uchumi wa Bluu na Masuala ya Bahari wa Kenya, amesema katika hotuba yake ya ufunguzi kwamba nchi hiyo inatambua uwezo wa sekta mbalimbali ndani ya uchumi wa bluu, ikiwa ni pamoja na usafiri wa baharini na wa meli za mizigo, utalii, utamaduni na burudani, uvuvi na ufugaji wa samaki, nishati mbadala, na utafutaji wa viumbe hai majini ambao unaweza kuleta utajiri wa maana.

      "Uwekezaji katika uchumi wa bluu wa Afrika ni muhimu kwa ajili ya kufikia manufaa kama vile kupunguza umaskini na ukosefu wa usawa na kufikia maendeleo makubwa zaidi ya kijamii na kiuchumi," Mvurya amesema.

      Amependekeza kuwa mashirika ya uwekezaji katika uchumi wa bluu yanatakiwa kufadhili utafiti na uvumbuzi ambao utachochea ujasiriamali pamoja na minyororo mbalimbali ya thamani katika sekta ya uchumi wa bluu.

      Picha hii iliyopigwa Septemba 20, 2023, ikionyesha Kituo cha Mafuta cha Kenya Mombasa, huko Mombasa, Kenya. (Kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China / Xinhua)

      Takwimu zilizotolewa na Umoja wa Afrika zimeonesha kuwa, uchumi wa bluu wa bara hilo kwa sasa unaleta mapato yenye thamani ya dola takriban bilioni 300 za Kimarekani kila mwaka na kudumisha nafasi za ajira milioni 50. Umoja wa Afrika umekadiria kuwa uchumi wa bluu utafikia dola zaidi ya bilioni 405 za Marekani kwa mwaka na kutoa nafasi za ajira milioni 57 ifikapo Mwaka 2030.

      (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)