Timu ya Afrika yajiunga na “ligi kuu ya vijiji” ya China kwa lengo la kuhimiza mabadilishano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 13, 2024

Wachezaji wa Afrika kutoka Timu ya Soka ya Jumuiya ya Watu wa Liberia wakisalimiana na watazamaji wakati wa Ligi Kuu ya Vijijij huko Rongjiang. (Picha na Wang Bingzhen/Xinhua)

Wachezaji wa Afrika kutoka Timu ya Soka ya Jumuiya ya Watu wa Liberia wakisalimiana na watazamaji wakati wa Ligi Kuu ya Vijijij huko Rongjiang. (Picha na Wang Bingzhen/Xinhua)

Mechi ya soka ya kirafiki kati ya Timu ya Soka ya Jumuiya ya Watu wa Libera na Timu ya Soka ya Liaoning Donggang ilivutia ufuatiliaji mkubwa kwenye Ligi Kuu ya Vijiji ya China katika Wilaya ya Rongjiang, Mkoa wa Guizhou mapema mwezi huu.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa timu ya Afrika kushiriki kwenye ligi hiyo, ambayo inajulikana kama “Cunchao” kwa Lugha ya Kichina.

Ligi hiyo imeanza kupata ufuatiliaji mkubwa katika za nchi za Afrika, zikiwemo Benin na Afrika Kusini. Ukaribu kati ya “Cunchao” na Afrika umesababisha kuanza kwa urafiki kati ya kijiji kidogo cha Rongjiang na timu ya Afrika, na kuanzia mwaka huu, mechi za kimataifa zimefanyika katika uwanja wa Ligi Kuu ya Vijiji.

Siku moja kabla ya mchezo, timu hiyo ya wanajumuiya wa Liberia ilitembelea Kijiji cha Dali cha Kabila la Wadong huko Rongjiang, kujionea utamaduni wake wa kikabila na kuimba nyimbo pamoja na wanakijiji.

“Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kujionea utamaduni wa kabila la Wadong, hali ambayo ni ya kipekee sana. Watu katika kijiji hicho walikuwa wa kirafiki, na niligusiwa sana,” anasema Godrich Samwely, mwanafunzi kijana wa chuo, akiongeza kuwa kama angepata fursa angependa kutembelea tena Rongjiang.

“Hii ilikuwa safari ya soka na urafiki,” anasema Jose Jacobs, ambaye amekuwa akicheza soka kwa zaidi ya miaka 20.

Mwishoni mwa Machi, kwenye uwanja wa soka wa Kijiji cha Belle Cite nchini Benin, timu 12 za vijiji zilizindua toleo la kwanza la “Ligi Kuu ya Vijiji ya Afrika”, ambayo hufanyika wakati wa wikendi na imepangwa kuendela hadi mwisho wa mwezi huu.

Washangiliaji wakileta vitafunio kwenye uwanja wa soka wakati wa Ligi Kuu ya Viijiji huko Rongjiang, Mkoa wa Guizhou, China mapema mwezi huu. (Picha na Wang Bingzhen/Xinhua)

Washangiliaji wakileta vitafunio kwenye uwanja wa soka wakati wa Ligi Kuu ya Viijiji huko Rongjiang, Mkoa wa Guizhou, China mapema mwezi huu. (Picha na Wang Bingzhen/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha