China yasema kuongeza ushuru kwa bidhaa za China kutaleta hasara kubwa kwa kampuni na wanunuzi wa Marekani

人民网

      (Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 16, 2024

      BEIJING - Marekani imefanya makosa zaidi katika kuendelea kuingiza siasa katika masuala ya biashara na kuongeza ushuru kwa bidhaa za China, hatua ambazo zitaleta hasara kubwa zaidi kwa kampuni na wanunuzi wa Marekani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema Jumatano.

      Wang ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari alipoulizwa kutoa maoni yake kuhusu hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru hivi karibuni kwa magari yanayotumia umeme ya China na bidhaa nyinginezo.

      Amesisitiza kuwa Marekani imefanya makosa zaidi katika kuongeza ushuru huo na kuendelea kwake kuingiza siasa katika masuala ya biashara. "Hii itaongeza tu gharama za bidhaa zinazoagizwa kutoka nje kwa kiasi kikubwa, kusababisha hasara kubwa kwa kampuni na wanunuzi wa Marekani, na hata kulazimisha wanunuzi wa Marekani kulipa zaidi."

      Moody's (kampuni ya kimataifa ya Ukadiriaji wa mambo ya fedha) imekadiria kuwa asilimia 92 ya ushuru zinazoongezeka zitaangukia wanunuzi wa Marekani, huku wastani wa matumizi ya kaya ya Marekani utaongezeka kwa dola 1,300 za Marekani kila mwaka, Wang amesema, akiongeza kuwa hatua za kujilinda kibiashara za Marekani zitaleta athari kubwa kwa usalama na utulivu wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na usambazaji.

      "Tumeona kwamba viongozi kadhaa wa kisiasa wa Ulaya wamesema kwamba kuhusu mambo ya ushuru, ni wazo baya kuvuruga biashara ya dunia," amesema.

      “China inaitaka Marekani iheshimu kanuni za WTO kwa makini na kuondoa ushuru huo wa ziada mara moja,” amesema, huku akisisitiza kuwa China itachukua hatua zote zinazohitajika kulinda haki na maslahi yake.

      (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)