Mahakama ya Umoja wa Mataifa yasikiliza ombi la Afrika Kusini dhidi ya operesheni za Israel huko Gaza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 17, 2024
Mahakama ya Umoja wa Mataifa yasikiliza ombi la Afrika Kusini dhidi ya operesheni za Israel huko Gaza
Wawakilishi wa Israel wakionekana kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) katika Jumba la Amani huko The Hague, Uholanzi, Mei 16, 2024. (Picha na Sylvia Lederer/Xinhua)

THE HAGUE, Uholanzi - Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imefungua usikilizaji wa kesiwa siku mbili siku ya Alhamisi kuhusu ombi la Afrika Kusini la kusitisha mashambulizi ya kijeshi ya Israel huko Gaza ambapo Balozi wa Afrika Kusini nchini Uholanzi Vusimuzi Madonsela amewaambia majaji kuwa nchi yake imerejea mahakamani "kutokana na Wapalestina wanaendelea kuuawa, mpaka sasa zaidi ya 35,000 hadi sasa wameuawa, na sehemu kubwa ya Gaza ikiwa imgeuzwa vifusi."

"Israel inaendelea kudharau maisha ya Wapalestina, ikifanyika bila kujali sheria na kuwajibika," amesema, huku akielezea sababu ya Afrika Kusini kuendelelea kutoa wito wa kulinda "haki za kimsingi za watu wa Palestina."

Tangu maombi yake ya kwanza kwa ICJ Desemba 29, 2023, Afrika Kusini imetuma maombi ambatanishi Februari na Machi 2024 kwa "hatua za muda" za kukomesha "vitendo vinavyoendelea vya mauaji ya halaiki ya Israeli dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza."

Katika ombi hilo lililotolewa tena, Balozi Madonsela amesisitiza kuongezeka kwa "hali mbaya ya Gaza" na "kuharibiwa kwa Gaza kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu Vita vya Pili vya Dunia."

Madonsela ameitaka mahakama hiyo kuiamuru Israel kusitisha operesheni zake za kijeshi huko Gaza, pamoja na Rafah, na kuondoa wanajeshi wake katika Ukanda wote wa Gaza.

Zaidi ya hayo, balozi huyo ametoa wito kwa Israel kuchukua "hatua zote zinazofaa" ili kuhakikisha ufikiaji wa Umoja wa Mataifa na misaada ya kibinadamu kwa Gaza bila vikwazo.

Hoja ya Israel itawasilishwa kwa ICJ leo Ijumaa, huku hukumu ikitarajiwa kutolewa katika wiki zijazo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha