Kituo cha Utafiti cha Volkswagen Mkoani Anhui nchini China chaonyesha matumaini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 17, 2024
Kituo cha Utafiti cha Volkswagen Mkoani Anhui nchini China chaonyesha matumaini
Picha iliyopigwa Mei 16, 2024 ikionyesha njia ya ya majaribio yenye mfano wa mijini ya Kampuni ya Teknolojia ya Volkswagen China (VCTC) huko Hefei, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (Xinhua)

HEFEI - Kampuni ya Teknolojia ya Volkswagen nchini China (VCTC), ambayo ni kituo kikubwa zaidi cha utafiti cha Kundi la Kampuni za Magari za Volkswagen nje ya Ujerumani, imefanya hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa awamu ya Tatu ya kituo hicho na kuzindua Njia ya Majaribio yenye mfano wa Mjini (CTT) siku ya Alhamisi huko Hefei, mji mkuu wa Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China.

Ukiwa na eneo lenye ukubwa wa mita za mraba takriban 110,000, mradi huo wa awamu ya Tatu umepangwa kukamilika ifikapo Mwaka 2027, huku karakana yake ya majaribio ikitarajiwa kuanza kutumika ifikapo Mwaka 2025.

Kituo hicho kilichopanuliwa cha utafiti kitawezesha kazi ya utafiti kwenye majukwaa ya magari yanayotumia nishati mpya (NEV), kuunda magari kikamilifu, sehemu na vifaa, pamoja na uunganishaji na majaribio ya vifaa na mifumo, kwa mujibu wa VCTC.

CTT inajikita katika upimaji wa ufanisi na uthibitishaji wa ufanisi wa magari yaliyounganishwa na teknojia za kisasa, na kuifanya kuwa njia ya kwanza ya majaribio ya Kundi la Kampuni za Volkswagen nchini China.

Ikichukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba karibu 200,000, CTT ina vifaa mbalimbali na njia za kufanyia majaribio. Baada ya kufanya kazi kikamilifu, wahandisi wa utafiti wanaweza kufanya majaribio ya wakati halisi na marekebisho kwenye miundo mpya ya magari, kuharakisha kasi ya kurudia ya uendelezaji wa mifumo na vifaa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha