-
China yarusha satelaiti ya mawasiliano kwa ajili ya Pakistan
XICHANG - China imerusha kwa mafanikio satelaiti ya mawasiliano ya kazi mbalimbali kwa ajili ya Pakistan kwa kutumia roketi ya Long March-3B kwenye Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Xichang katika mkoa wa Sichuan kusini magharibi mwa China majira ya saa 2:12 usiku wa siku ya Alhamisi. Satelaiti hiyo imeingia kwenye obiti yake iliyopangwa. Urushaji huo ni safari ya 524 ya mfululizo wa roketi za Long March.
31-05-2024
-
BYD yatoa Toleo la 5 la gari linalotumia teknolojia ya nishati mchanganyiko ya DM
Watu wakitembelea banda la Kampuni ya magari ya BYD kwenye maonyesho ya magari huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Mei 1, 2024. (Xinhua/Zhang Bowen) SHENZHEN – Kampuni kubwa ya China ya kuzalisha magari yanayotumia nishati mpya (NEV) ya BYD imetoa toleo la 5 teknolojia ya nishati mchanganyiko ya DM (dual mode) kwa magari ya kutumia nishati mchanganyiko za mafuta na betri ya kuchajiwa ambayo yanaweza kuendesha kwa umbali wa kilomita 2,100 baada ya kuchajiwa. Kwa teknolojia
30-05-2024
-
Wanaanga wa China wa Chombo cha Shenzhou-18 wakamilisha kazi yao ya kwanza ya kutembea kwenye anga ya juu
BEIJING – Wanaanga wa China wa chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-18 walioko kwenye kituo cha anga ya juu cha China wamekamilisha kazi yao ya kwanza ya kutembea kwenye anga ya juu saa 12:58 jioni (Kwa saa za Beijing) siku ya Jumanne, Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limesema. Ye Guangfu, Li Cong na Li Guangsu wamefanya kazi kwa saa takriban nane na nusu katika kukamilisha majukumu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ufungaji wa vifaa vya kulinda vifusi angani, na wamesaidiwa na mkono wa roboti
29-05-2024
-
Eneo la kujionea na kujaribu ana kwa ana teknolojia za kisasa la Mkutano wa 7 wa China ya Kidijitali lafunguliwa Fujian
Mkutano wa 7 wa China ya Kidijitali utafanyika Fuzhou, Mkoa wa Fujian, Kusini-Mashariki mwa China kuanzia leo Mei 24 hadi 25. Eneo la kujionea na kujaribu ana kwa ana teknolojia za kisasa la Mkutano huo, linalochukuka eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 56,000, likijumuisha sehemu kuu tano, limefunguliwa katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na Maonyesho cha Fuzhou Strait siku ya Alhamisi.
24-05-2024
-
‘Wahusika wa Filamu ya Transformers’ wabadilisha taaluma mjini Chongqing, China na kuunda magari!
Timu ya utafiti na mahojiano ya Gazeti la People’s Daily Online ya "Songa China" ya Chongqing imeingia katika kiwanda cha magari cha Chang’an cha Liangjiang, China, Mei 20. Katika kiwanda hicho, michakato muhimu inafanyika kiotomatiki kwa asilimia 100, na bidhaa zake zinauzwa sehemu mbalimbali duniani. Timu hiyo ipo tayari, ikiwa na data thabiti na hamasa kazini. Ninahisi hali ya teknolojia na siku za baadaye inayoletwa na "uzalishaji bidhaa" na "uzalishaji bidhaa kwa kutumia teknolojia za kisas
23-05-2024
-
Intaneti ya kasi ya satelaiti ya obiti ya chini ya China yatumika nje ya nchi kwa mara ya kwanza
Roketi ya Long March-2C iliyobeba satelaiti ya majaribio ya teknolojia za intaneti ya satelaiti ikirushwa kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China, Desemba 30, 2023. (Picha na Wang Jiangbo/Xinhua) BEIJING - Kampuni ya kibinafsi ya anga ya juu ya China, kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Thailand, imefanya jaribio la kwanza la mtandao wa mawasiliano ya intaneti ya kasi ya satelaiti ya obiti ya chini kwa mafanikio nchini Thailand. Mafanikio hayo yanaashiria mat
22-05-2024
-
Video: Roboti za viwandani zaonesha mdundo wa kipekee
Roboti za viwandani zenye hakimiliki ya kujitegemea kikamilifu ya China zikifanyiwa majaribio kwenye karakana ya kampuni ya roboti ya SINSUN, mjini Shenyang, Mkoa wa Liaoning, China, Tarehe 14, Mei. Bofya video, na utahisi mdundo pamoja na timu ya mahojiano ya "China Kusonga Mbele" ya People's Daily Online.
15-05-2024
-
China yaharakisha mageuzi ya kidijitali katika sekta ya uzalishaji viwandani
Picha ya kumbukumbu ikionyesha Kituo cha Pili cha Uzalishaji wa Hali ya Juu cha NIO huko Hefei, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (Xinhua) BEIJING - China imeanza kufanya juhudi kubwa zaidi katika mageuzi ya kidijitali ya sekta ya uzalishaji viwandani ili kukuza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora na kuimarisha kasi ya ukuaji wa uchumi wake. Baraza la Serikali la China kwenye mkutano wake wa utendaji hivi karibuni lilipitisha mpango wa utekelezaji unaolenga kuendeleza mambo ya kidijitali
14-05-2024
-
Mkoa wa Qinghai wa China wazindua mradi wa umeme wa 750-kV unaounganisha nishati mbadala kwenye gridi
Picha iliyopigwa Mei 7, 2024 ikionesha mradi wa kupitisha na kupoza umeme wa 750-kV katika Wilaya ya Gonghe, Mkoa wa Qinghai wa China. (Picha na Dong Qingfang/Xinhua) Mradi wa kupitisha na kupoza umeme wa 750-kV umekamilika na kuanza kufanya kazi katika Mkoa wa Qinghai, Kaskazini Magharibi mwa China, imesema Kampuni ya Nishati ya Umeme wa Gridi ya Taifa ya China tawi la Qinghai. Mradi huo ulio kwenye mwinuko wa mita 3,175 juu ya usawa wa bahari katika Wilaya ya Gonghe ya mkoa huo utasaidia kuung
14-05-2024
-
Kiwanda cha Mimea: Uwanja mpya wa Uzalishaji wa Kilimo
Mfumo wa uzalishaji wa mimea wenye ufanisi wa hali ya juu, ambapo mazingira ya ukuaji wa mimea yanawezesha kufikia udhibiti kamilifu kwa kutumia akili mnemba, umetumika katika kiwanda cha mimea cha kiotomatiki cha kikazi kipya katika Mkoa wa Fujian, China. Katika kiwanda hicho cha mimea, kilimo cha mboga hakihitaji jua na udongo. Kwa sasa mazao ya kila siku ya mboga yanaweza kufikia tani 1.5, na usambazaji endelevu wa mazao umefikiwa katika maeneo ya karibu kama vile miji ya Fuzhou, Xiamen na Qu
13-05-2024