Biashara ya kijani ya China yatoa ufundi na kipato cha kudumu kwa vijana wa Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 14, 2024

Picha iliyopigwa Mei 2, 2024 inaonesha boda-boda zinazotumia umeme zikioneshwa kwenye Kampuni ya Teknolojia ya Nishati Mpya ya Hanlin Africa huko Nairobi, Kenya. (Xinhua/Li Yahui)

Picha iliyopigwa Mei 2, 2024 inaonesha boda-boda zinazotumia umeme zikioneshwa kwenye Kampuni ya Teknolojia ya Nishati Mpya ya Hanlin Africa huko Nairobi, Kenya. (Xinhua/Li Yahui)

Kwa mikogo ya kujiamini, Moses Kimani alikuwa akizungumza na wateja kwenye lango la kuingia kwenye Kampuni ya Teknolojia ya Nishati Mpya ya Hanlin Africa, ambayo ni kampuni ya China inayoshughulika na uunganishaji wa sehemu na uuzaji wa vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme iliyoko Kusini mwa mji wa Nairobi, Kenya.

Kijana huyo wa miaka 27 aliyesomea masomo ya jiografia na mazingira ya asili ana hamasa ya kuwaeleza wenzake kwa nini wanatakiwa kuchagua vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme.

Kimani alijiunga na kampuni ya Hanlin Africa karibu miaka miwili iliyopita na ari yake kubwa ya kunadi magari yanayotumia umeme pamoja na boda-boda na tuk-tuk zinazotumia umeme nchini Kenya haina mpinzani, akitaka kuleta mageuzi ya vyombo vya usafiri nchini Kenya, kukabiliana na utoaji wa kaboni, na kutoa kazi za kijani kwa vijana.

“Usafiri wa vyombo vinavyotumia umeme unawasaidia vijana; una uwezo mkubwa katika siku za baadaye. Bidhaa zetu zimevutia uhitaji mkubwa kwa soko hapa,” Kimani ameliambia shirika la habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni kwenye mstari wa kuunganisha sehemu za vyombo vya usafiri wa kampuni ya Hanlin Africa.

Hanlin Africa ilianzisha biashara yake nchini Kenya Machi 9, 2023. Kampuni hiyo ina waajiriwa wenyeji zaidi ya 30, wakiwemo wafanyakazi zaidi ya 20 wa mstari wa mbele.

Kimani ambaye ni mkuu wa masoko amesema kuwa, wakati wa kufanya kazi amepata ujuzi muhimu kutoka kwa wasimamizi wake wa China, kama vile kuwasiliana na wateja, nidhamu na stadi za biashara.

Amesema kuwa waendeshaji wa boda-boda, ambao wengi wao ni vijana, wana shauku ya kuhamia kwenye matumizi ya boda-boda zinazotumia umeme ili kupunguza bili za mafuta na kusaidia mageuzi ya usafiri wa kijani ya nchi hiyo.

Irene Mutie mwenye umri wa miaka 24 aliyesoma masomo ya mauzo na masoko ambaye kwa sasa ni mwakilishi wa mauzo wa Hanlin Africa, amesema ikilinganishwa na waajiri wake wa zamani, kampuni hiyo ya China inahamisha ujuzi wa kiufundi kwa vijana wenyeji.

“Ufundi ambao tumepata hadi sasa ni mzuri. Tunaweza kuona namna boda-boda zinazotumia umeme zinavyounganishwa sehemu zake. Tumejifunza pia umuhimu wa nidhamu na kuheshimu wengine,” amesema Mutie.

Mutie ameeleza kuwa, katika siku za baadaye, kwa usafiri wa vyombo vinavyotumia umeme kunufaisha kundi muhimu la vijana wenyeji, serikali inapaswa kutunga sera na sheria za uungaji mkono ili kuhimiza uwekezaji katika sekta hiyo.

Moses Kimani akiongea wakati wa mahojiano na shirika la habari la China, Xinhua huko Nairobi, Kenya Mei 2, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

Moses Kimani akiongea wakati wa mahojiano na shirika la habari la China, Xinhua huko Nairobi, Kenya Mei 2, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

Mfanyakazi akiunganisha vifaa na sehemu za boda-boda inayotumia umeme kwenye bohari la Hanlin Africa huko Nairobi, Kenya Mei 2, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

Mfanyakazi akiunganisha vifaa na sehemu za boda-boda inayotumia umeme kwenye bohari la Hanlin Africa huko Nairobi, Kenya Mei 2, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

Wateja wakijaribu boda-boda inayotumia umeme kwenye kampuni ya Hanlin Africa huko Nairobi, Kenya, Mei 2, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

Wateja wakijaribu boda-boda inayotumia umeme kwenye kampuni ya Hanlin Africa huko Nairobi, Kenya, Mei 2, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha