Shirikisho la Wazalishaji Magari la China lalaani kujilinda kibiashara kwa Marekani katika sekta ya magari ya kutumia nishati mpya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 14, 2024

Watu wakitembelea maonyesho la magari huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi Kaskazini-Magharibi mwa China, Mei 1, 2024. (Xinhua/Zhang Bowen)

Watu wakitembelea maonyesho la magari huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi Kaskazini-Magharibi mwa China, Mei 1, 2024. (Xinhua/Zhang Bowen)

BEIJING - Shirikisho la Wazalishaji Magari la China (CAAM) limelaani Marekani kutia chumvi juu ya wasiwasi wa uzalishaji kupita mahitaji halisi ya soko na hofu ya usalama wa taifa kuhusu sekta ya magari yanayotumia nishati mpya ya China likiuelezea kuwa ni mfano wazi wa kujilinda kibiashara.

Fu Bingfeng, naibu mkuu na katibu mkuu mtendaji wa CAAM, amesisitiza kuwa hatua kama hizo za kujilinda na kujitenga "hazipaswi kuwa mada" ya sekta ya magari ya kutumia nishati mpya.

Fu ameyasema hayo wakati ambapo kuna ripoti ya ushuru mpya kwa magari yanayotumia umeme ya China uliopangwa na Marekani.

Fu amesema, tunahitaji kuwa na upeo wa dunia nzima na ufunguaji mlango ili kuhimiza maendeleo yenye nguvu ya utengenezaji wa magari, huku akisisitiza ahadi ya China ya kufungua mlango kwenye kiwango cha juu, na hii italeta fursa kubwa za soko kwa kampuni za magari za dunia nzima. CAAM hivi majuzi ilitoa seti ya kwanza ya matokeo ya ukaguzi kuhusu uchakataji wa data ya gari, ikithibitisha kufuata viwango vya usalama wa data kwa modeli 76 za magari katika kampuni sita, ambazo ni, BYD, Li Auto, Lotus, Hozon New Energy, Tesla na NIO.

Fu amesisitiza umuhimu wa uchakataji salama wa data ya magari kama kigezo kipya cha kuendeleza magari ya kisasa, huku akibainisha kuwa CAAM inafuata kanuni ya kuhudumia kwa usawa wadau wote wa ndani na nje ya China.

"Tesla, kampuni pekee ya magari inayowekezwa kwa mtaji wa kigeni katika seti hii ya matokeo ya ukaguzi, imeshiriki kikamilifu kwani inatambua mwelekeo wa watumiaji wa siku zijazo wa magari ya kujiendesha yenyewe katika soko kubwa la China," Fu amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha