Bandari ya Biashara Huria ya Hainan yapata oda ya kwanza ya matengenezo ya ndege kutoka Korea Kusini

人民网

      (Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 15, 2024

      Mfanyakazi wa kampuni ya matengenezo ya Ndege ya Grand China (GCAM) akifanya kazi ndani ya chumba cha abiria cha ndege iliyoingia China kwenye sehemu ya maegesho ya ndege ya kituo cha matengemezo ya ndege huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Mei 13, 2024. (Xinhua/Zhang Liyun)

      Ndege aina ya Boeing 737-800 ya Shirika la Ndege la Jeju la Korea Kusini hivi karibuni imefanyiwa matengenezo na kampuni ya matengenezo ya ndege ya Grand China (GCAM), ambayo pia ni oda ya kwanza ya matengenezo ya ndege zinazoingia nchini China kutoka Korea Kusini katika Bandari ya Biashara Huria ya Hainan, China.

      Huduma hiyo inatarajiwa kuendelea kwa siku takriban 16, zinazostahili kupata upendeleo katika bandari hiyo ya biashara huria ikiwa ni pamoja na kusamehewa amana ya pesa taslimu pamoja na mafuta na matengenezo bila kutozwa ushuru.

1/6