Biden na Trump wakubali kufanya duru mbili za mdahalo wa uchaguzi wa urais

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 16, 2024

Picha iliyopigwa Arlington, Virginia, Marekani Oktoba 22, 2020 ikionyesha matangazo ya moja kwa moja ya kituo cha televisheni cha C-SPAN ya Rais wa Marekani Donald Trump (Kulia) na mpinzani wake wa chama cha Democrat Joe Biden wakiwa kwenye mdahalo wao wa mwisho kwenye uchaguzi wa urais wa Mwaka 2020. (Xinhua/Liu Jie)

Picha iliyopigwa Arlington, Virginia, Marekani Oktoba 22, 2020 ikionyesha matangazo ya moja kwa moja ya kituo cha televisheni cha C-SPAN ya Rais wa Marekani Donald Trump (Kulia) na mpinzani wake wa chama cha Democrat Joe Biden wakiwa kwenye mdahalo wao wa mwisho kwenye uchaguzi wa urais wa Mwaka 2020. (Xinhua/Liu Jie)

WASHINGTON - Rais Joe Biden wa Marekani na Rais wa zamani Donald Trump, ambao ni wagombea wa urais walioteuliwa katika vyama vya Democrat na Republican nchini Marekani, wamekubaliana siku ya Jumatano kufanya duru mbili za mdahalo ya kampeni mwezi Juni na Septemba.

Duru hiyo mbili za mdahalo kati ya Biden na Trump itaandaliwa na vituo viwili vya televisheni vya CNN na ABC, mtawalia.

"Nimepokea na kukubali mwaliko kutoka @CNN kwa ajili ya mdahalo wa tarehe 27 Juni. Kwako wewe, Donald. Kama ulivyosema: popote, wakati wowote, mahali popote," amesema Biden katika video fupi iliyochapishwa kwenye Mtandao wa X, ambao zamani ulijulikana kwa jina la Twitter, huku akiongeza kuwa pia" amepokea na kukubali mwaliko wa mdahalo utakaoandaliwa na ABC Septemba 10."

"Donald Trump alifaulu mara mbili za mdahalo Mwaka 2020. Tangu wakati huo, hajajitokeza kwa mdahalo. Sasa anajifanya kama anataka kufanya mdahalo nami tena. Naam, nafurahi, rafiki," Biden amesema.

Trump pia amethibitisha kwamba atafanya midahalo na Biden katika mara mbili katika mwezi wa Juni na Septemba, huku akiongeza kwamba anapendekeza kufanya midahalo zaidi ya duru mbili.

Kwa mujibu wa CNN, mdahalo huo utafanyika katika studio za kituo hicho zilizoko Atlanta bila watazamaji. ABC pia imeripoti kwamba Biden na Trump wamekubali kufanya mjadala wakati wa watazamaji wengi katika studio zake.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha