Rais Xi Jinping afanya mkutano maalum na Rais Putin uliofanyika Zhongnanhai, Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 17, 2024

Rais wa China Xi Jinping akifanya mkutano maalumu na Rais wa Russia Vladimir Putin  katika Zhongnanhai mjini Beijing, China, Mei 16, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

Rais wa China Xi Jinping akifanya mkutano maalumu na Rais wa Russia Vladimir Putin katika Zhongnanhai mjini Beijing, China, Mei 16, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya mkutano maalum na Rais wa Russia Vladimir Putin siku ya Alhamisi katika Zhongnanhai mjini Beijing, ambapo wamekuwa na mazungumzo ya kina kuhusu masuala ya kimkakati yanayofuatiliwa na pande zote. Rais Xi ameeleza kuwa Dunia inapitia mabadiliko ambayo hayajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita na kuingia kipindi kipya cha misukosuko na mageuzi. Katika kukabiliana na hali hiyo ya Dunia inayoendelea kubadilika ikiwa na kuyumba na misukosuko, China imedumisha dhamira yake ya kimkakati.

Amesema chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, watu wa China wameshinda matatizo na changamoto mbalimbali, na wanajitahidi kuhimiza maendeleo yenye sifa bora na ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

Rais Xi amesema, China ingependa kushirikiana na Russia na nchi nyingine katika kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kuelekeza usimamizi wa dunia kwenye mwelekeo sahihi, kulinda kwa pamoja haki na usawa wa kimataifa, na kuhimiza amani ya dunia na maendeleo kwa pamoja.

Rais Putin amesema kuwa, maendeleo ya China hayazuiliki na kwamba hakuna nguvu inayoweza kuzuia ukuaji na maendeleo ya China, Russia iko tayari kuboresha ushirikiano na China na nchi nyingine za Dunia ya Kusini ili kuhimiza haki na usawa wa kimataifa, na kuijenga dunia iwe na usawa zaidi na ncha nyingi.

Viongozi hao wawili wa nchi pia wamekuwa na mazungumzo ya kina kuhusu mgogoro wa Ukraine.

Rais Xi amefafanua msimamo thabiti wa China na juhudi za kuhimiza suluhu ya kisiasa ya suala la Ukraine, huku akisisitiza kwamba ili kushughulikia suala lolote kubwa, ni muhimu kushughulikia dalili na chanzo cha msingi, na kupanga mipango ya sasa na vile vile ya muda mrefu.

Amesema China inaunga mkono kuitishwa kwa mkutano wa kimataifa wa amani unaotambuliwa na Russia na Ukraine kwa wakati ufaao kwa ushiriki sawa na majadiliano ya haki ya machaguo yote, ili kusukuma mbele suluhu ya kisiasa ya suala la Ukraine, na China iko tayari kuendelea kufanya kazi ya kiujenzi katika suala hili.

Putin amefahamisha maoni na misimamo husika ya Russia, akisema kuwa Russia inathamini msimamo usio na upendeleo, wa haki na usawa wa China kuhusu suala la Ukraine na anaikaribisha China kuendelea kuonesha umuhimu wake wa kiujenzi katika suluhu ya kisiasa ya suala hilo.

Rais wa China Xi Jinping akifanya mkutano maalumu na Rais wa Russia Vladimir Putin  katika Zhongnanhai mjini Beijing, China, Mei 16, 2024. (Xinhua/Ju Peng)

Rais wa China Xi Jinping akifanya mkutano maalumu na Rais wa Russia Vladimir Putin katika Zhongnanhai mjini Beijing, China, Mei 16, 2024. (Xinhua/Ju Peng)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha