Marais wa China na Russia wahudhuria ufunguzi wa shughuli ya “Miaka ya Utamaduni ya China na Russia”

人民网

      (CRI Online) Mei 17, 2024

(Picha na Gao Jie/Xinhua)

(Picha na Zhang Ling/Xinhua)

(Picha na Liu Weibing/Xinhua)

      Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin wamehudhuria ufunguzi wa shughuli ya “Miaka ya Utamaduni ya China na Russia” na tafrija ya kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia Alhamisi mjini Beijing.

      Akibainisha kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, Rais Xi amesema historia ya uhusiano huo katika miaka 75 iliyopita inaonyesha kwamba kuimarisha na kuendeleza ujirani mwema na urafiki wa kudumu, uratibu wa kimkakati wa pande zote, na ushirikiano wa kunufaishana vinatumikia masilahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili na watu wake, na kuendana na matarajio ya jumuiya ya kimataifa na mwelekeo wa nyakati, ambao una umuhimu usioweza kubadilishwa.

      Kufanya shughuli ya mwaka yenye kaulimbiu maalumu katika kila nchi ni desturi nzuri ya mabadilishano kati ya watu na ya kiutamaduni kati ya China na Russia, vilevile ni mambo maalumu na ya kielelezo katika historia ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, ambao unakaribishwa sana na watu wa nchi hizo mbili.

      Rais Xi amesema kuwa, inaaminika kuwa kauli mbiu hiyo itaongeza msukumo mpya katika kuendeleza urafiki kati ya China na Russia kutoka kizazi hadi kizazi na kuongeza maelewano na kujenga uhusiano wa karibu kati ya watu wake.

      (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)