Kenya, Uganda zafikia makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili

人民网

      (Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 17, 2024

      Rais William Ruto wa Kenya (katikati) akimkaribisha mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) katika Ikulu mjini Nairobi, Kenya, Mei 16, 2024. (Picha na Fred Mutune/Xinhua)

      NAIROBI - Kenya na Uganda zimetia saini makubaliano mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbili siku ya Alhamisi ambapo moja ya makubaliano hayo yanaruhusu Uganda kuagiza na kusafirisha bidhaa za mafuta yaliyosafishwa kupitia Kenya kutoka kwa nchi wazalishaji, ili kutatua changamoto zinazokabili sekta ya mafuta ya Uganda, kwa mujibu wa Rais wa Kenya William Ruto.

      "Tuna imani kwamba makubaliano hayo yataimarisha uhusiano wetu thabiti na kuuweka kwenye mkondo wa mageuzi," Rais Ruto amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni aliyekuwa ziarani Kenya.

      Ruto pia amesema, anaangazia umuhimu wa kurefusha reli ya Kenya ya standard gauge (SGR) kutoka Naivasha hadi Kampala, Uganda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kama njia endelevu na bora ya miundombinu kwa usafirishaji wa bidhaa.

      Nchi zote mbili zimeagiza mawaziri wao kukusanya rasilimali kwa ajili ya mradi huu na kuripoti maendeleo ifikapo mwishoni mwa Mwaka 2024.

      Zaidi ya hayo, Kenya imeahidi kushirikiana kwa karibu na Uganda katika kushughulikia changamoto za kiusalama katika kanda hiyo, ikiwa ni pamoja na Sudan, Sudan Kusini, Somalia na DRC.

      (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)