-
Jeshi la Sudan lahamisha waumini 6 wa kanisa katoliki wa Italia kutoka KhartoumKHARTOUM - Jeshi la Sudan (SAF) limetangaza siku ya Jumanne kuwahamisha waumini sita wa kanisa katoliki wa Italia na raia 20 wa Sudan Kusini ambao walikuwa wamekwama kusini mwa Khartoum tangu kuzuka kwa vita mwezi Aprili mwaka jana. "SAF na Idara kuu ya Ujasusi (GIS) imehamisha watawa watano wa Jumuiya ya Wakatoliki wa Italia, kasisi kutoka Jumuiya ya Don Bosco ya Italia, na raia 20 wa Sudan Kusini kutoka kusini mwa Khartoum," Nabil Abdalla, msemaji wa SAF amesema katika taarifa. Watu hao walioh
07-08-2024
-
Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Misri wafanya mazungumzo kuhusu hali ya Mashariki ya Kati
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Misri Badr Abdelatty siku ya Jumanne. Katika mazungumzo hayo, Wang amesema chini ya mwongozo wa kimkakati wa marais wa nchi hizo mbili, ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Misri umepata maendeleo makubwa, na upo katika kipindi bora zaidi katika historia. Pande hizo mbili pia zimebadilishana mawazo kuhusu hali ya Mashariki ya Kati. Wang amesema mauaji dhidi ya kiongozi mkuu wa kundi la
07-08-2024
-
Rais wa Zambia atoa wito wa kufanyika makubaliano ya kimataifa kumaliza mgogoro kati ya Russia na Ukraine
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ametoa wito wa kuwepo kwa maelewano ya haraka ya kimataifa ili kumaliza mgogoro kati ya Russia na Ukraine. Amesema hayo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Ivanovych Kuleba ambaye anatembelea nchini Zambia. Amesema kuwa mgogoro wa Russia na Ukraine unahitaji kutatuliwa kwa njia za amani, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa ili kuongeza hali ya utulivu na amani katika eneo hilo. Aidha ametoa wito wa kuimarishwa kwa uhusiano wa pand
07-08-2024
-
Niger yatangaza kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine “mara moja”
Msemaji wa serikali ya kijeshi ya Niger Amadou Abdramane Jumanne ametangaza kupitia televisheni ya kitaifa akisema, Niger itavunja uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine “mara moja”. Kwenye taarifa yake amesema, wanachukua hatua hiyo kutokana na kitendo cha Ukraine cha “kuunga mkono makundi ya kigaidi”, na kutoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufanya uamuzi juu ya “uvamizi” wa Ukraine. Siku mbili zilizopita, serikali ya mpito ya Mali ilitangaza kuwa itavunja uhusiano wa kidiplomasia
07-08-2024
-
Kenya yasema mkutano ujao wa FOCAC utaimarisha uhusiano kati yake na China
Mkuu wa mawaziri wa Kenya ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora, Musalia Mudavadi amesema mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wa 2024 (FOCAC) uliopangwa kufanyika Septemba mjini Beijing, utaongeza uhai katika uhusiano wa pande mbili kati ya China na Kenya ambao umedumu kwa zaidi ya miongo sita. Akiongea kwenye mkutano na wawakilishi kutoka jumuiya za Wachina huko Nairobi, Mudavadi ameelezea matarajio ya nchi hiyo kwa mkutano huo ujao, katika uhusiano wake wa kidip
07-08-2024
-
Vitu katika Bandari ya Sudan vyasubiri ruhusa ya kupelekwa kwenye kambi iliyokumbwa na njaa huko Darfur Kasakazini
Afisa wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu amesema siku ya Jumanne kuwa vitu vya msaada vya kuokoa maisha tayari viko katika bandari kuu ya Sudan kwa ajili ya kupelekwa kwenye kambi ya Zamzam huko Darfur Kaskazini, ambako awali maafisa walitangaza kuwa kuna hali ya njaa. Hata hivyo, Mkurugenzi wa Operesheni na Utetezi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), Edem Wosornu amesema shehena hiyo ikiwa na vitu kama vile dawa muhimu, vifaa vya lishe,
07-08-2024
-
Chebet wa Kenya ashinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 5000 kwa wanawake katika Michezo ya Olimpiki ya Paris
Mkenya Beatrice Chebet alifanya umalizaji wa kishindo ili kushinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 5000 kwa wanawake katika Michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Jumatatu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alivuka mstari wa mwisho wa mbio hizo kwa kumaliza mbio kwa dakika 14 sekunde 28.56, zaidi ya sekunde mbili mbele ya bingwa mtetezi Sifan Hassan wa Uholanzi, ambaye amepata medali ya fedha. Nadia Battocletti wa Italia amepata medali ya shaba kwa kumaliza mbio kwa dakika 14 sekunde 31.
07-08-2024
-
China yatoa wito kwa ICC kuheshimu kikamilifu mamlaka ya mahakama na masuala halali ya Sudan
UMOJA WA MATAIFA - Dai Bing, naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumatatu kuheshimu kikamilifu mamlaka ya mahakama na masuala halali ya Sudan wakati wa kushughulikia kesi ya Darfur. "China imekuwa ikifuatilia kwa karibu uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kuhusu hali ya Darfur," amesema Balozi Dai katika hotuba yake kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ICC Sudan. Balozi Dai a
06-08-2024
-
Kampuni za Tanzania na China zasaini mradi wa uchimbaji madini ya chuma wenye thamani ya dola milioni 77 za kimarekani
Shirika la Taifa la Maendeleo la Tanzania (NDC) na kampuni ya Hexingwang ya Fujian, China zimesaini makubaliano, ili kuendeleza mradi wa uchimbaji wa chuma wa Maganga Matitu katika mkoa wa Njombe. Hafla ya utiaji saini wa mradi huo wenye thamani ya dola milioni 77.4 za Kimarekani utakaozalisha chuma cha sifongo kama malighafi kwa viwanda vya chuma imeshuhudiwa na Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Bw. Doto Biteko jijini Dar es Salaam. Akitoa hotuba fupi baada ya makuba
06-08-2024
-
Wasomali wafanya maandamano dhidi ya al-Shabab baada ya shambulizi kali la kwenye hoteli
Mamia ya Wasomali, wakiwemo maafisa wakuu wa serikali, wamefanya maandamano ya amani mjini Mogadishu, Somalia, ili kulaani kundi la mrengo wenye itikadi kali za dini la al-Shabab kufuatia shambulizi kali la kwenye hoteli ya Lido Beach View lililosababisha vifo vya watu 37. Wakikusanyika katika eneo la hoteli hiyo, waandamanaji walikuwa wamebeba mabango ya kuipinga al-Shabab na kulaani ukatili wa kundi hilo. Huku wakitamka kauli mbiu za kukemea na kuchukizwa na al-Shabab, waandamanaji hao pia wal
06-08-2024