Reli ya China-Laos yarahisisha usafirishaji wa matunda

人民网

      (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 12, 2024

      Picha hii iliyopigwa tarehe 8 Oktoba 2023 ikionyesha treni ya kwanza ya mizigo ya Shanghai-Kunming Lancang-Mekong Express ikiondoka katika Stesheni ya Reli ya Wangjiaying Magharibi huko Kunming, Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Hu Chao)

      KUNMING - Reli ya China-Laos imesafirisha tani zaidi ya laki moja za matunda mwaka huu hadi kufikia Alhamisi, ikiwa ni ongezeko la karibu asilimia 120 mwaka hadi mwaka, mamlaka ya reli ya China imesema.

      Siku ya Alhamisi, shehena yenye uzito wa tani 108 ya matunda ya duriani kutoka Thailand iliyosafirishwa kupitia Reli ya China-Laos ilipakuliwa kwenye bandari ya kimataifa ya usafirishaji ya Kunming Hongyun, ikizidi kiwango cha tani 100,000.

      Imechukua saa 29 pekee kwa shehena hiyo ya matunda kufika eneo la upakuaji huko Kunming, mji mkuu wa Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China, kutoka stesheni ya reli ya Vientiane Kusini, Shirika la Reli la China Tawi la Kunming limesema.

      Kutokana na hatua zilizoratibiwa za uidhinishaji wa forodha, matunda ya kitropiki kutoka Asia Kusini na Asia Kusini Mashariki yanaendelea kusafirishwa hadi China kupitia reli hiyo.

      Kwa sasa, muda kuidhinisha vibali vya forodha vya kuvuka mpaka kupitia reli hiyo umepunguzwa hadi muda usiopungua saa tano, ikiwezesha usafirishaji wa matunda na mboga mboga, maua na bidhaa nyingine zinazohitaji usafiri wa haraka, limesema kundi hilo.

      Reli kati ya China na Laos, ambayo ni mradi kinara wa ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, ilianza kufanya kazi Desemba 2021. Reli hiyo yenye urefu wa kilomita 1,035 inaunganisha mji wa Kunming nchini China na ule wa Vientiane nchini Laos.

      (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)