China yapiga hatua kubwa katika kuendeleza maendeleo ya Teknolojia ya 5G

人民网

      (Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 07, 2024

      Watu wakitazama trekta inayotumia teknolojia ya haidrojeni ya 5G+ inayojiendesha bila dreva kwenye Maonyesho ya 13 ya Uwekezaji na Biashara ya Maeneo ya Kati ya China (Maonyesho ya Maeneo ya Kati ya China 2024) mjini Changsha, Mkoa wa Hunan, Katikati ya China, Mei 31, 2024. (Xinhua/Chen Sihan)

      BEIJING – Siku ya Alhamisi ilikuwa inatimia mwaka wa tano tangu kutolewa kwa kundi la kwanza la leseni za Teknolojia ya 5G kwa matumizi ya kibiashara nchini China, na mpaka hivi leo vituo zaidi ya milioni 3.7 vya msingi vya 5G vimefungwa sehemu mbalimbali nchini, matumizi makubwa ya 5G nchini China yamenufaisha watu na biashara, yakileta urahisi na fursa muhimu.

      Ufuatao ni ukweli wa mambo na takwimu muhimu kuhusu maendeleo ya 5G nchini China.

      Kwanza, Aprili 2020, Kampuni ya China Mobile ilianzisha kituo cha msingi cha 5G kwenye sehemu yenye mwinuko wa mita 6,500 ya Mlima Qomolangma, ambacho ndicho kituo cha msingi cha 5G chenye urefu wa juu zaidi duniani.

      Pili, Juni 2020, China ilikamilisha ujenzi wa mtandao wake wa kwanza wa chini ya ardhi wa 5G katika Mkoa wa Shanxi, na kuweka rekodi ya kuwa mtandao wa chini ya ardhi zaidi wa 5G duniani.

      Tatu, hadi sasa, matumizi ya 5G yamefungamana na viwanda na mashirika 71 kati ya 97 vilivyo muhimu vya kiuchumi nchini, na miradi zaidi ya 94,000 ya kuifanya 5G kuwa ya kibiashara imezinduliwa.

      Nne, China ina watumiaji zaidi ya milioni 800 wa simu za mkononi za 5G kwa sasa, ikichukua asilimia zaidi ya 52 ya simu zote duniani.

      Tano, China inalenga kujenga viwanda 10,000 vya 5G katika kipindi cha Mpango wa 14 wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021-2025).

      Sita, Machi 2024, Kampuni ya China Mobile ilizindua mtandao wa kwanza wa kibiashara wa 5G-A huko Hangzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China.

      Wataalamu walisema, ingawa changamoto zinaendelea katika mageuzi kutoka 5G hadi 6G, kila mafanikio mapya ya kiteknolojia na uvumbuzi wa programu utafungua uwezekano mpya kwa sekta ya baadaye na kuongeza matarajio ya maisha ya kisasa. 

      (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)