Katika Picha: Mandhari ya Kivutio cha Utalii cha Shibaozhai huko Chongqing, Kusini Magharibi mwa China

人民网

      (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 12, 2024

      Watu wakitembelea eneo la Shibaozhai lenye kivutio cha utalii katika Wilaya ya Zhongxian ya Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China Julai 10, 2024. (Xinhua/Huang Wei)

      Kivutio cha utalii cha Shibaozhai kinaonekana kama bonsai yenye umbo la moyo iliyoko katikati ya sehemu ya Magenge Matatu ya Mto Changjiang wa China. Kwenye sehemu hiyo kuna pagoda ya mbao yenye ghorofa 12 na urefu wa mita 56 ambayo inasimama juu ya nguzo 20 na kuegemea miamba iliyo karibu na mto huo. Ujenzi wa pagoda hiyo ulianzia Enzi ya Ming (1368-1644) ya China katika zama za kale, na pagoda hiyo ni sehemu ya kivutio kikuu cha utalii kwenye eneo la Shibaozhai. 

1/10