Malipo rahisi ya kutumia simu za mkononi yaleta tajiriba bora ya safari kwa watalii wa kigeni nchini China

人民网

      (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2024

      Mfanyakazi akiwapa watalii wa kigeni data ya maelezo kuhusu namna ya kutoa malipo katika Mji wa Tianjin, Kaskazini mwa China, Aprili 7, 2024. (Xinhua/Sun Fanyue)

      BEIJING - Kwa Jamie na Liliana, wanandoa waliosafiri hadi Mji wa Chengdu Kusini-Magharibi mwa China kutoka Australia, kutoa malipo kwa kutumia programu ya simu ya mkononi ya Alipay ni majaribio maalum kama kutembea kwenye Mtaa wa Kuanzhai wa Chengdu wenye historia ndefu ulio na njia pana au nyembamba zenye vivutio mbalimbali.

      "Malipo yamefanyika kwa haraka sana. Ni rahisi sana," amesema Liliana, ambaye kwa kawaida anaposafiri anatoa malipo kwa kutumia pesa taslimu au kwa kadi za malipo.

      Liliana ni miongoni mwa watembeleaji wengi wa kigeni nchini China ambao wamenufaika na ahadi ya China ya kutoa urahisi kwa watalii wa kigeni wakati wa kutoa malipo katika safari yao.

      Miaka mingi ya ukuaji wa kasi imeifanya China kuwa kinara katika malipo ya kutumia simu. Kiwango cha kufikika kwa malipo ya kutumia simu nchini China kilifikia asilimia 86, ambacho ni kiwango cha juu zaidi duniani, hadi kufikia mwisho wa Mwaka 2023.

      Hata hivyo, kutoa malipo kwa kutumia simu pia kunaleta vizuizi kwa wasafiri wa kigeni wanaotembelea China kwa mara ya kwanza. Watembeleaji China wa kigeni wanaotegemea kadi za benki na pesa taslimu wanaweza kukumbwa na matatizo wakati wa mchakato wa kutoa malipo, kwa kuwa wachuuzi wa mitaani au watoa huduma wadogo wanapendelea malipo ya kutumia simu kuliko kutoa pesa taslimu au kwa kadi za malipo za kimataifa.

      Kwa kutilia maanani jambo hili, serikali ya China imeanzisha hatua nyingi za kusaidia watalii wa kigeni kufurahia mazingira ya kutoa malipo bila usumbufu nchini China sawa na yale yanayofurahiwa na wenyeji.

      Shukrani kwa njia hiyo ya kutoa malipo iliyorahisishwa kwa simu za mkononi kwa watalii wa kigeni nchini China kama Liliana sasa wanaweza kuunganisha kadi za benki za ng'ambo kwa urahisi kwa kutumia Alipay au Tenpay, programu mbili kuu za malipo nchini China.

      Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, idadi ya miamala ya kadi za kigeni kupitia majukwaa hayo ya malipo ya kutumia simu za mkononi iliongezeka mara 6.65 kutoka mwaka mmoja uliopita hadi kufikia milioni karibu 37.4, na jumla ya kiasi cha miamala kiliongezeka mara 8.03 hadi kufikia yuan bilioni 5.42 (dola za Kimarekani kama milioni 760.29) kwa mujibu wa takwimu kutoka kampuni ya China ya kuruhusu miamala mtandaoni ya NetsUnion Clearing.

      Leo, watalii wa kigeni zaidi wanafurahia tajiriba ya kusafiri na kuzunguka China kwenye simu ya mkononi.

      (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)