-
Hohhot, Mji maarufu wa kihistoria wa China kwenye Njia ya Kale ya kusafirisha Chai
Mji wa Hohhot wa Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, China uliokaribia Mlima Daqing upande wa kaskazini na kukaribia Mto Manjano upande wa kusini, historia ya ujenzi wake imekuwa na zaidi ya miaka 2,400. Mji wa Hohhot uko kwenye njia muhimu ya usafirishaji tangu enzi za kale. Wakati wa Enzi za Ming na Qing, ulikuwa kituo cha kijeshi na kibiashara na makutano muhimu ya mjini kwenye Njia ya Kale ya Farasi kusafirisha Chai (Tea Horse Road). Mawasiliano na Mafungamano katika tamaduni za mbugani
30-07-2024
-
Magofu ya Mji wa Kale wa Gedi nchini Kenya Yaorodheshwa kwenye Orodha ya Mali ya Urithi wa Dunia ya UNESCO
Mkutano wa 46 wa Mali ya Urithi wa Dunia wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) uliofanyika New Delhi, India, hivi karibuni umepitisha azimio la kuyaingiza magofu ya mji wa kale wa Gedi nchini Kenya kwenye Orodha ya Mali ya Urithi wa Dunia ya UNESCO. Mji huo wa kale wa Gedi, ulioko katika eneo la pwani ya Kenya, Kaunti ya Kilifi, ni mabaki ya mji wa Waswahili. Magofu yaliyopo sasa ya mji huo wa kale wa Gedi yamezungukwa na misitu minene ya asili, yakiendelea kuwa
29-07-2024
-
Sanaa za Mikono za kale zaoneshwa kwenye Jumba la Makumbusho la Sanxingdui mkoani Sichuan, China
Maonesho yaliyopewa jina la “Ufundi wa Sanaa za Mikono na Ustadi: Kuonesha Mafanikio ya Uhifadhi na Urejeshaji tena wa Mabaki ya kale ya Kiutamaduni yaliyofukuliwa hivi karibuni kutoka Eneo la Kihistoria la Sanxingdui” yamefunguliwa mkoani Sichuan, China siku ya Jumanne. Zaidi ya kazi 50 zilizorejeshwa upya katika hali ya awali za vyombo vya shaba, vyombo vya dhahabu, vyombo vya jade, vyombo vya meno ya ndovu na mabaki mengine ya kale zinaoneshwa katika maonesho hayo, ambayo yataendelea hadi mwi
24-07-2024
-
Watalii wavutiwa na utamaduni wa Dunhuang kupitia teknolojia ya kidijitali
Maonyesho ya kidijitali yanayotumia teknolojia ya 3D na vifaa VR yanafanyika ili kusaidia watalii kufurahia utamaduni wa Dunhuang katika Mkoa wa Gansu, Kaskazini-Magharibi mwa China. Ikiwa ni moja ya malango muhimu ya kuingia kwenye Njia ya Kale ya Hariri, Dunhuang ni sehemu iliyopo Mapango ya Mogao, ambayo ni Eneo la Urithi wa Dunia wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) linalojivunia mkusanyiko mkubwa wa kazi za sanaa za Kibuddha.
23-07-2024
-
Kijiji kidogo cha Watu wa kabila la Wamiao chahimiza ustawishaji na maendeleo zaidi ya kijiji
Kijiji cha Wuying katika eneo la mpaka kati ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini-Magharibi mwa China na Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, kikiwa na historia ya zaidi ya miaka 200, ni kijiji kidogo cha watu wa Kabila la Wamiao, ambacho kiko kwenye eneo la milima mirefu inayovuka mpaka kati ya mikoa ya Guangxi na Guizhou. Hapo awali, milima na mazingira magumu yasiyoweza kupitika yaliwafanya wenyeji wa huko kuwa maskini sana. Katika miaka ya hivi karibuni, Kiji
19-07-2024
-
Waandaaji wasema Tamasha la ZIFF kuvutia filamu zaidi ya 3,000 kutoka duniani kote
Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF), ambalo pia linajulikana kama Tamasha la Nchi za Majahazi, litakuwa na filamu zaidi ya 3,000 kutoka kote duniani. Hayo yamesemwa na afisa mtendaji mkuu wa ZIFF Joseph Mwale kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika Jumanne jijini Dar es Salaam. Amesema tamasha hilo ambalo ni tukio kubwa la kitamaduni la Zanzibar litakalofanyika kuanzia Agosti 1 hadi 4, litavutia watengeneza filamu kutoka nchi 100, zikiwemo China, Tanzania, Ujerumani, Uingereza, In
18-07-2024
-
Maonyesho makubwa kuhusu ustaarabu wa kale wa Misri yafunguliwa Shanghai
SHANGHAI - Maonyesho makubwa ya ustaarabu wa kale wa Misri, ambayo ni makubwa zaidi ya aina yake kufanyika nje ya Misri katika miaka 20 iliyopita, yamefunguliwa siku ya Jumatano mjini Shanghai, mashariki mwa China ambapo mabaki ya kale jumla ya 788 kutoka Misri, pamoja na mabaki ya kale ya China, yanaonyeshwa kwenye Jumba la Makumbusho la Shanghai, yakiwapa watembeleaji wake uhondo wa sanaa kutoka kwenye ustaarabu huo wa kale. Maonyesho hayo, "Kilele cha Piramidi: Ustaarabu wa Misri ya Kale" yam
18-07-2024
-
Baraza la uhifadhi wa kidijitali wa mali ya urithi wa kitamaduni lafunguliwa Beijing
Wageni wakihudhuria mkutano wa saba wa Baraza la Kimataifa la Uhifadhi wa Kidijitali wa Mali ya Urithi wa Kitamaduni mjini Beijing, China, Julai 16, 2024. (Xinhua/Fang Sixian) Mkutano wa saba wa Baraza la Kimataifa la Uhifadhi wa Kidijitali wa Mali ya Urithi wa Kitamaduni (CHCD) chini ya mada ya "Weka Sura Mpya: Uvumbuzi wa Teknolojia Wahimiza Uhifadhi wa Kidijitali wa Mali ya Urithi", limeanza Jumanne mjini Beijing, ambapo mikutano miwili itafanyika sambamba ambayo itafuatilia zaidi teknolojia
17-07-2024
-
Habari picha: Uchoraji wa picha ndani ya chupa huko Kunming, Mkoa wa Yunnan wa China
Uchoraji wa picha ndani ya chupa ndogo ni aina ya sanaa ya jadi ya China. Hapo awali ilihusisha chupa ndogo za ugoro ambazo zilikuwa na picha zilizochorwa na Maandiko ya Kichina yaliyoandikwa ndani ya chupa. Uchoraji huo wa picha unafanyika kwa kupenyeza brashi maalum kupitia mdomo wa chupa. Mchakato wa uchoraji, ambao hufanyika kwa kuijongesha brashi kabisa ndani ya chupa, ambapo mchoraji atatakiwa kuchora picha kwa usahihi kabisa. Sun Hongyan, mchoraji mwenye umri wa miaka 49, amechora picha m
17-07-2024
-
Jumba la Makumbusho ya makaburi ya chini ya ardhi kwenye Njia ya kale ya Hariri lafunguliwa Xinjiang
URUMQI – Katika sehemu ya mita takriban nane chini ya mtaa wenye maduka mengi wa Mji wa Kuqa, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, Kaskazini-Magharibi mwa China, kuna makaburi ambayo yamefunikwa tuli chini ya ardhi kwa zaidi ya miaka 1,700. Hata hivyo, leo makaburi hayo, ambayo kihistoria yanaanzia kwenye Njia ya Kale ya Hariri, yamefukuliwa na kuoneshwa kwenye Jumba la Makumbusho la kipekee. Jumba hilo la makumbusho la chini ya ardhi la Makaburi ya Kale ya Enzi za Wei na Jin (220-420) limefung
16-07-2024